July 03, 2025
press_release
Hukumu ya Mahakama ya Juu Yatuza Zinaa (Uasherati) Sawa na Ndoa
Mahakama ya Juu imeamua kwamba watoto waliozaliwa nje ya ndoa kwa wazazi Waislamu wanastahili kurithi mali ya baba yao, ambayo inawakilisha maendeleo muhimu katika tafsiri ya sheria ya Kiislamu ya kibinafsi nchini Kenya. Hii ilikuja baada ya Mahakama ya Juu, siku ya Jumatatu, Juni 30, kukataa rufaa iliyowasilishwa na Fatima Othman Aboud Faraj, ambaye alitaka kuwatenga watoto wa mumewe marehemu, Salim Juma Hakim Kitendo, kutoka kwenye urithi wake kwa madai kwamba walizaliwa nje ya mfumo wa ndoa ya Kiislamu inayotambuliwa.